MATUMIZI YA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA MFUMO WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI TANZANIA: MJADALA WA MWEGAMO NA MAWANDA YAKE
Abstract
Makala hii ni sehemu ya ripoti ya mradi wa utafiti mpana uliofanyika mwaka 2018/19 katika mikoa mitano ambayo ni Lindi, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Kagera na Kaskazini Pemba. Utafiti huo ulifadhiliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma. Utafiti ulihusu suala la matumizi ya lugha ya Kiswahili katika duara zima la utoaji wa huduma za afya. Watoa taarifa katika utafiti huu walikuwa: wanataaluma wa taaluma za afya, watoa huduma, wapewa huduma na viongozi wa sekta ya afya. Data zilikusanywa kupitia njia za udodosaji, usaili, na mijadala ya vikundi lengwa. Makala hii inahusu mwegamo wa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania pamoja na mawanda yake. Makala ina sehemu nne mbazo ni: Utangulizi, mwegamo wa matumizi ya Kiswahili katika utoaji wa huduma za afya, mawanda ya matumizi ya Kiswahili katika utoaji wa huduma za afya pamoja na hitimisho.