UFUTUHI WA KIAFRIKA: NADHARIA MPYA YA KUSHUGHULIKIA TAALUMA ZA KI-INSIA

Authors

  • Athumani S. Ponera

Abstract

Makala hii inawasilisha jaribio la kuifafanua nadharia ya Ufutuhi wa   Kiafrika kama nadharia mpya yenye uwezo wa kutumika kushughulikia masuala ya ki-insia. Taaluma za ki-insia, katika makala hii, zinamaanisha shughuli kama vile tafiti na tahakiki zinazofanywa kwenye nyuga zinazohusiana na lugha, sanaa, historia, falsafa, na utamaduni. Kwa kipindi kirefu, taaluma kama hizi zinazowahusu Waafrika zimekuwa zikishughulikiwa kwa kutumia viunzi vya nadharia vyenye asili na mwegamo wa maeneo ya nje ya jamii za Kiafrika. Hali hii, kwa namna moja au nyingine, husababisha upungufu katika kupata majibu ya matatizo yanayoshughulikiwa. Katika kuitikia wito kwa wanataaluma wa Kiafrika kutafuta na kutumia nadharia zenye asili na mwegamo wa jamii husika, makala hii inaitambulisha dhana ya Ufutuhi wa Kiafrika kama nadharia yenye uwezo wa kuwa Kiunzi cha Nadharia8 chenye uwezo wa kuendeshea taaluma za ki-insia.

Downloads

Published

2021-10-05

How to Cite

Ponera, A. S. (2021). UFUTUHI WA KIAFRIKA: NADHARIA MPYA YA KUSHUGHULIKIA TAALUMA ZA KI-INSIA. JARIDA LA MNYAMPALA, 2(1), 134–143. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/12

Issue

Section

ARTICLES