USAWIRI CHANYA WA WATOTO KATIKA FASIHI YA WATOTO KAMA NJIA FAAFU YA KUJENGA JAMII BORA YA LEO NA KESHO: MIFANO KUTOKA VITABU TEULE VYA WATOTO VYA KISWAHILI

Authors

  • Leonard H. Bakize

Abstract

Mshengyezi (2003) anadai kuwa, fasihi siyo tu matokeo ya matendo ya wanajamii, bali pia, ni wakala mzuri wa kuipa jamii mwelekeo mzuri kama ikisawiri mambo vizuri na ikatumiwa vizuri. Memmi (2006) anasisitiza kuwa waandishi wa fasihi wana chombo muhimu sana mikononi mwao ambacho kutokana na ubunifu wao, huwawezesha wasomaji kuamini na kuathirika kutokana na kile wanachokisoma au kusikiliza. Memmi (keshatajwa) anaongeza kuwa hata kama kazi fulani ya fasihi ni ya kubuni, bado wahusika wake wanaweza kubebeshwa mawazo ya waandishi kuhusiana na jinsi ambavyo wasanii huyaona maisha na jinsi wanavyotamani maisha hayo yawe. Hivyo, yeye anahitimisha kwa kusema kuwa, fasihi ni chanzo muhimu sana cha ujenzi wa taifa endelevu. Lengo huu la makala hii ni kushadidia hoja kwamba, fasihi ya watoto ikiwasawiri vyema watoto na kuwaonesha kuwa ni watu muhimu, tunaweza kuwa na jamii bora leo na kesho. Makala inachambua na kubainisha hoja zake kwa kutumia kazi kumi na moja za Kiswahili zilizoandikwa kwa ajili ya kusomwa na watoto. Makala inaongozwa na Nadharia za Usimulizi na Kisosholojia. Katika matokeo ya uchambuzi wa data, inabainika kwa uwazi kwamba, watoto wanaposoma, huamini yale wanayoyasoma; hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kubadilishwa na kile wanachokisoma. Hivyo, kama tukichukua tahadhari tukawasawiri vyema watoto, kama asemavyo Memmi (2006), tunayo nafasi kubwa ya kuwaathiri vizuri watoto ili wajenge jamii nzuri.

Downloads

Published

2021-10-05

How to Cite

Bakize, L. H. (2021). USAWIRI CHANYA WA WATOTO KATIKA FASIHI YA WATOTO KAMA NJIA FAAFU YA KUJENGA JAMII BORA YA LEO NA KESHO: MIFANO KUTOKA VITABU TEULE VYA WATOTO VYA KISWAHILI. JARIDA LA MNYAMPALA, 2(1), 83–94. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/5

Issue

Section

ARTICLES