NGONJERA NA MTAZAMO MPYA WA MALEZI YA WATOTO NA VIJANA

Authors

  • Shadidu Abdallah Ndossa Chuo Kikuu cha St John’s cha Tanzania

Abstract

Malezi ya watoto na vijana kwa jumla ni ada muhimu katika ustawi wa jamii yoyote inayohitaji kupiga hatua za kimaendeleo. Isivyo bahati, jamii imeshughulishwa mno masuala mengine ya kimaisha, na kuwaacha watoto na vijana wajilee wenyewe. Wakati haya yakitokea, waandishi wawili— Ramadhan Nyembe na Abdallah Seif—wanajitokeza kuikumbusha jamii kuhusu ulezi wa watoto na familia kupitia ngonjera. Makala hii inachambua mchango wa wasanii hawa wa ngonjera katika kuirejesha jamii katika mstari wa malezi kupitia tungo zao mbili, Ngonjera Elimishi Na.1 na Ngojera: Nasaha na Uzalendo. Uchambuzi wa matini umetumika kama njia ya kupata taarifa mbalimbali za kitabuni. Aidha, nadharia ya uhalisia imetuongoza katika uchambuzi na uwasilishaji wa taarifa mbalimbali za kitabuni. Hii ni kusema kuwa, mambo mengi yaliyozungumzwa na waandishi ni mwangwi wa maisha halisi yanayojitokeza katika jamii. Ili kufikia lengo la makala hii, mwandishi ameshughulikia ngonjera zinazohusiana na malezi ya watoto na vijana tu. Kwa jumla, wasanii wameweza kufikisha ujumbe muhimu kwa jamii. Wamezungumzia mambo muhimu kama vile umuhimu wa elimu kwa watoto, madhara ya pombe na dawa za kulevya, imani za kishirikina na heshima kwa wakubwa.

Downloads

Published

2020-06-30

How to Cite

Ndossa, S. A. (2020). NGONJERA NA MTAZAMO MPYA WA MALEZI YA WATOTO NA VIJANA. JARIDA LA MNYAMPALA, 1(1), 132–145. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/40

Issue

Section

ARTICLES