MATATIZO YA UFUNDISHAJI WA SINTAKSIA KATIKA VYUO VIKUU NCHINI TANZANIA

Authors

  • Kulikoyela K. Kahigi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Fabiola Hassan Chuo Kikuu cha Dodoma

Abstract

Kuanzia miaka ya mwishoni mwa karne ya 20 hadi leo, ufundishaji wa sintaksia umekumbwa na matatizo makuu mawili: (1) nadharia za kufundisha, na (2) maarifa na stadi ambazo mhitimu wa shahada ya kwanza anapaswa kuwa nazo. Makala hii inajadili matatizo haya katika muktadha wa ufundishaji wa sintaksia katika Idara za Kiswahili, vyuo vikuu vya Tanzania. Makala inajadili matatizo haya kwa kuhusisha pia changamoto ya uchanganyaji wa mikabala ya ufundishaji. Katika kujadili matatizo haya yote, makala inabainisha kwamba changamoto hizi za ufundishaji wa sintaksia zinatokana na sababu kuu mbili: (1) uhaba wa wataalamu wa sintaksia katika ngazi husika; na (2) kukosekana kwa jukwaa au “chombo” kinachoweza kusimamia mijadala kuhusu nadharia, mikabala na maarifa yanayopaswa kuzingatiwa katika ufundishaji wa sintaksia/isimu kwenye vyuo vikuu. Miongoni mwa mapendekezo yanayotolewa ni kuwapo kwa chombo cha uratibu kitakachosimamia ufundishaji wa isimu ya Kiswahili katika vyuo vikuu, si nchini Tanzania tu, bali kwenye vyuo vikuu vyote vya Afrika Mashariki. Kwa kuwa tayari kuna vyombo kadhaa (kama vile CHAKAMA-TZ na TATAKI), kimojawapo cha vyombo hivyo kinaweza kupewa jukumu hilo kama ikionekana inafaa.

Downloads

Published

2020-06-30

How to Cite

Kahigi, K. K. ., & Hassan, F. . (2020). MATATIZO YA UFUNDISHAJI WA SINTAKSIA KATIKA VYUO VIKUU NCHINI TANZANIA. JARIDA LA MNYAMPALA, 1(1), 105–121. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/38

Issue

Section

ARTICLES