UTAMADUNI WA MZANZIBARI: MILA NA DESTURI KATIKA VAZI LA KANGA

Authors

  • Saade S. Mbarouk Chuo kikuu cha SUMAIT
  • Ulfat A. Ibrahim Chuo kikuu cha SUMAIT

Abstract

Makala hii inaangazia matumizi ya vazi la kanga katika mila na desturi katika utamaduni wa Mzanzibari. Kila jamii huwa na kaida zake ambazo hutofautiana na jamii nyingine. Kaida hizo huwa katika chakula, mavazi, pamoja na mfumo mzima wa maisha. Lengo la makala hii ni kubainisha kwa namna gani Wazanzibari wanavyotumia kanga kulingana na mila na desturi zao. Matumizi hayo huwa katika hatua mbalimbali za makuzi ya mwanadamu, kuanzia kuzaliwa kwake, kuishi na kufa kwake. Makala hii ni sehemu ya utafiti mkubwa uliofanywa na Saade Mbarouk (2011) ambao unahusu Athari za Semi za Kanga kwa Jamii ya Zanzibar. Ukusanyaji wa data ulifanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano. Nadharia ya Naratolojia imetumika katika kuchambua data. Katika makala hii waandishi wameeleza fasili ya kanga, aina za kanga, asili ya jina la kanga pamoja na historia ya kanga. Mwisho, wameelezea umuhimu wa kutunza utamaduni wa jamii.

Downloads

Published

2020-06-30

How to Cite

Mbarouk, S. S., & Ibrahim, U. A. . (2020). UTAMADUNI WA MZANZIBARI: MILA NA DESTURI KATIKA VAZI LA KANGA. JARIDA LA MNYAMPALA, 1(1), 26–37. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/32

Issue

Section

ARTICLES