FASIHI YA KISWAHILI: MUSTAKABALI WA TANZANIA KATIKA MUKTADHA WA UTANDAWAZI

Authors

  • Gerephace Mwangosi Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha
  • Mussa, E. Msamilah Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha

Abstract

Wanazuoni wengi wa ndani na nje ya Afrika wanatumia mbinu mbalimbali za kisanaa ili kueleza masuala yanayosawiri hali halisi iliyopo katika mataifa yao. Baadhi ya masuala yanayoelezwa ni pamoja na kutamalaki kwa utandawazi na athari zake katika mataifa yanayoendelea. Makala hii imeeleza nafasi ya fasihi ya Kiswahili katika kuimarika kwa utandawazi katika nchi za Kiafrika kwa kipindi cha miongo mitatu iliyopita. Katika kipindi hiki, mataifa ya Kiafrika yameshuhudia mapinduzi makubwa katika mifumo ya siasa na sera za uchumi huria unaodhibitiwa na mataifa ya kibepari. Kwa hiyo, makala hii imechunguza athari za utandawazi nchini Tanzania kwa kurejelea riwaya teule za Bina-Adamu (2002) ya K. W. Wamitila na Msomi Aliyebinafsishwa (2012) ya N. Nyangwine. Riwaya hizi zimeteuliwa kwa kuwa zinaakisi vizuri hali halisi ya harakati na athari za utandawazi hapa nchini. Pia, inadokeza mustakabali wa Tanzania ya sasa na ijayo. Data za makala hii zilipatikana maktabani. Nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchambuzi na mjadala wa data zilizowasilishwa. Makala inahitimisha kuwa kadiri harakati za utandawazi zinavyozidi kuimarika nchini, ndivyo mifumo ya kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi inavyozidi kudhoofika na kuporomoka.

Downloads

Published

2020-06-30

How to Cite

Mwangosi, G., & Msamilah, M. E. (2020). FASIHI YA KISWAHILI: MUSTAKABALI WA TANZANIA KATIKA MUKTADHA WA UTANDAWAZI. JARIDA LA MNYAMPALA, 1(1), 13–25. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/31

Issue

Section

ARTICLES