RIWAYA YA KISWAHILI: JICHO FICHUZI NA ANGAZI LA VIVUTIO VYA UTALII ZANZIBAR

Authors

  • Masoud Nassor Mohammed Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)
  • Geofrey Kitula King’ei Chuo Kikuu cha Kenyatta

Abstract

Lugha ya Kiswahili na fasihi yake zinajengana. Kukua kwa lugha ya Kiswahili kunaimarisha ukuaji wa fasihi ya Kiswahili. Kwa upande mwingine, kukua kwa fasihi ya Kiswahili kunaimarisha pia maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Kwa pamoja, maendeleo ya lugha ya Kiswahili na fasihi yake yanachangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa sekta ya utalii ambayo inachangia kukua kwa uchumi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Fasihi ya Kiswahili, hasa riwaya, ina mchango mkubwa katika kuvifichua, kuvionesha, kuvitangaza na kuvieleza vivutio vya utalii katika visiwa vya Zanzibar. Hatimaye, watalii wa ndani na nje ya nchi, hutembelea na kuchangia pato la taifa na la watu binafsi. Makala inaangalia namna baadhi ya riwaya za Kiswahili za Zanzibar zilivyoibua na kuvitangaza vivutio vya utalii visiwani Zanzibar na hatimaye kuimarika kwa uchumi wake. Data za makala imekusanywa kwa njia ya udurusu wa matini za riwaya teule nne: Kiu (1972), Asali chungu (1977), Vuta n’kuvute (1999), na Kosa la bwana Msa (1984). Nadharia ya uhalisia imetumiwa kuongoza uchambuzi wa data katika makala hii. Makala inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika fasihi ya Kiswahili na uimarishaji wa sekta ya utalii Afrika ya Mashariki hasa katika kipindi hiki cha hamasa ya uchumi wa buluu Zanzibar.

Downloads

Published

2023-05-31

How to Cite

Mohammed, M. N., & King’ei, G. K. (2023). RIWAYA YA KISWAHILI: JICHO FICHUZI NA ANGAZI LA VIVUTIO VYA UTALII ZANZIBAR. JARIDA LA MNYAMPALA, 3(1), 134–149. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/26

Issue

Section

ARTICLES