SUALA LA UPOLE KATIKA FASIHI ANDISHI: UCHANGANUZI KATIKA RIWAYA YA PENDO LA KARAHA

Authors

  • Agnes Mueni Muteti Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki
  • Evans M. Mbuthia Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Mary Ndung’u Chuo Kikuu cha Nairobi

Abstract

Makala hii inajadili suala la upole linavyojitokeza katika riwaya ya Pendo la karaha iliyoandikwa na John Habwe (2014). Misingi ya riwaya hii imejielekeza katika ukiukaji wa ukawaida ulioko katika jamii. Vijana wanatamani nafasi za kazi ughaibuni. Wanapofika huko, wanakumbana na changamoto nyingi na matarajio yao hayafikiwi. Kudra, bintiye Riziki na mhusika mkuu, anakata tamaa kutokana na kauli anazopokezwa na wanaomzunguka; naye Kassim anakata tamaa kutokana na vitendo anavyotendewa na mamaye, Rehema. Nadharia inayoongoza mjadala huu ni nadharia ya upole iliyoasisiwa na Brown & Levinson (1987). Makala inabainisha kauli zenye upole zinazotamkwa na wahusika mbalimbali, kuchunguza mikakati ya upole inayoteuliwa na wahusika katika mawasiliano yao na kutambua matendo yanayochangia kuwapo kwa upole katika mawasiliano baina ya wahusika. Kutokana na data zilizokusanywa, inaweza kuhitimishwa kuwa upole si suala la kiakademia tu, bali linaweza kuwa na umuhimu katika safu ya udiplomasia na katika masuala ya amani na maridhiano miongoni mwa wanajamii katika mataifa yetu na hata kimataifa.

Downloads

Published

2023-05-31

How to Cite

Muteti, A. M., Mbuthia, E. M., & Ndung’u, M. (2023). SUALA LA UPOLE KATIKA FASIHI ANDISHI: UCHANGANUZI KATIKA RIWAYA YA PENDO LA KARAHA. JARIDA LA MNYAMPALA, 3(1), 104–121. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/24

Issue

Section

ARTICLES