LUGHA MKAKATI KATIKA MAWASILIANO YA CHOKORAA

Authors

  • Ruth M. Binyanya Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Ayub Mukhwana Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Samuel M. Obuchi Chuo Kikuu cha Moi

Abstract

Makala hii inachunguza matumizi ya lugha mkakati katika mawasiliano ya chokoraa. Chokoraa huishi mitaani na hupitia changamoto mbalimbali zikiwamo unyanyapaa na ukosefu wa chakula. Kwa hali hii basi, chokoraa hufanya kazi kama vile kuwabebea wafanyabiashara wadogo bidhaa za kuuza na kuosha magari. Vile vile, chokoraa, wakati mwingine, huomba msaada kutoka kwa wanakundi-nje. Hali hizi mbalimbali ndizo huwafanya chokoraa kutumia lugha mkakati na kwa mitindo mbalimbali ili kutimiza nia zao za wakati husika. Data iliyokusanywa kuhusiana na mada hii inaonesha kuwa chokoraa hutumia lugha kutegemea muktadha wa mawasiliano. Tumebaini kuwa chokoraa hutumia lugha mkakati kwa kutumia mbinu kama vile kuchanganya ndimi, uradidi, matumizi ya majina yanayorejelea Mungu na vile vile matumizi ya lugha ya matusi kwa nia ya kupambana na unyanyapaa kutoka kwa wanakundi-nje. Kwa kufuata mkabala wa isimujamii, makala hii inaonesha kuwa chokoraa hutumia lugha mkakati ili kukidhi mahitaji yao ya wakati husika. Makala hii ni ya uchambuzi ubora na hivyo basi yalitumia data ambayo ilituwezesha kushughulikia mada hii. Data ambayo imetumiwa katika makala hii ilikusanywa na Ruth Binyanya baina ya Januari-Agosti, 2020 mtaani Mathare, jijini Nairobi kwa ajili ya tasnifu yake ya uzamivu ambapo alishughulikia matumizi ya lugha mkakati katika kutimiza nia mbalimbali za wanafamilia wa mitaani.

Downloads

Published

2023-05-31

How to Cite

Binyanya, R. M., Mukhwana, A., & Obuchi, S. M. (2023). LUGHA MKAKATI KATIKA MAWASILIANO YA CHOKORAA. JARIDA LA MNYAMPALA, 3(1), 72–87. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/22

Issue

Section

ARTICLES