UAINISHAJI WA MOFIMU KATIKA SENTENSI ZA KISWAHILI-KIINGEREZA

Authors

  • Shadrack Kirimi Nyagah Chuo Kikuu cha Chuka
  • Iribe Mwangi Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Basilio Gichobi Mungania Chuo Kikuu cha Nairobi

Abstract

Makala hii inalenga kuainisha mofimu katika sentensi zinazotokana na uhamishaji msimbo unaohusu lugha za Kiswahili na Kiingereza. Utafiti huu unaongozwa na Modeli  ya Kiunzi cha Lugha Msingi ya Myers-Scotton (1993) na modeli ya M-4 ya Myers- Scotton & Jake (2000). Kando na kuainisha mofimu katika sentensi za Kiswahili- Kiingereza, kazi hii pia inachunguza majukumu yanayotekelezwa na lugha za Kiswahili  na Kiingereza katika sentensi moja. Data ya utafiti huu imetokana na mazungumzo ya kawaida kutoka katika vipindi viwili vinavyoigizwa kwenye runinga ya NTV- Kenya ambavyo ni “The Wicked Edition” na “The Real Househelps of Kawangware.” Matokeo  ya uchunguzi huu yanadhihirisha kwamba mofimu katika sentensi za Kiswahili- Kiingereza zinaweza kuainishwa katika matapo manne makuu, yaani: mofimu za  kidhana, mofimu za kimfumo za mapema, mofimu mfumo za kidaraja na mofimu mfumo za nje. Kila aina ya mofimu hutekeleza jukumu mahususi. Hali kadhalika, lugha ya Kiswahili na ya Kiingereza huwa na uamilifu tofauti hivi kwamba lugha ya Kiswahili huitawala lugha ya Kiingereza kwa kuiwekea muundo wa kimofosintaksia ambamo mofimu za Kiingereza huchopekwa.

Downloads

Published

2023-05-31

How to Cite

Nyagah, S. K., Mwangi, I., & Mungania, B. G. (2023). UAINISHAJI WA MOFIMU KATIKA SENTENSI ZA KISWAHILI-KIINGEREZA. JARIDA LA MNYAMPALA, 3(1), 41–53. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/20

Issue

Section

ARTICLES