UCHANGANUZI WA UBADILISHAJI NA UCHANGANYAJI MSIMBO KATIKA NYIMBO ZA ASILI NCHINI TANZANIA: MIFANO KUTOKA KATIKA NYIMBO ZA KABILA LA WAMATENGO

Authors

  • Fokas Mkilima

Abstract

Makala hii inafafanua uchanganyaji msimbo na ubadilishaji msimbokatika nyimbo za asili ya kabila la Wamatengo nchini Tanzania. Kutokana na jamii nyingi kuwa na hali ya uwililugha au wingi lugha, mara nyingi, wazungumzaji huchagua msimbo wa kutumia kutegemeana na mazingira au sababu nyinginezo. Uchaguzi wa msimbo hupelekea wazungumzaji kuchanganya au kubadili msimbo. Makala hii inatokana na utafiti ulioongozwa na nadharia ya uwililugha. Jumla ya nyimbo 25 zilikusanywa na kufanyiwa uchunguzi. Pia, wahojiwa watano walishirikishwa ili kupata sababu za uchanganyaji na ubadilishaji msimbo katika nyimbo. Data zimewasilishwa kwa kila wimbo na kutolewa maelezo yanayofafanua vipengele vya uchanganyaji kama vile mofimu, maneno, virai, vishazi na sentensi pamoja na sababu za uchanganyaji au ubadilishaji huo.

Downloads

Published

2021-10-05

How to Cite

Mkilima, F. (2021). UCHANGANUZI WA UBADILISHAJI NA UCHANGANYAJI MSIMBO KATIKA NYIMBO ZA ASILI NCHINI TANZANIA: MIFANO KUTOKA KATIKA NYIMBO ZA KABILA LA WAMATENGO. JARIDA LA MNYAMPALA, 2(1), 65–82. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/2

Issue

Section

ARTICLES