CHANGAMOTO ZA UINGIZWAJI WA MASUALA YAHUSUYO LUGHA KATIKA SERA ZA ELIMU NA UTAMADUNI: HAJA YA KUWA NA SERA MAHUSUSI YA LUGHA TANZANIA

Authors

  • Ahmad Y. Sovu

Abstract

Makala hii inajadili changamoto mbalimbali zinazohusiana na sera ya lugha. Kwa muda mrefu, nchi ya Tanzania haina sera mahususi ya lugha, badala yake, masuala ya lugha yameingizwa katika Sera ya Utamaduni na Sera ya Elimu. Sera ya lugha ni jumla ya mawazo, matamko, sheria, kanuni na taratibu zenye kufafanua utekelezaji wa mabadiliko ya matumizi ya lugha (Mekacha, 2000; na Msanjila, 2009). Aidha, makala inafafanua kuhusu dhana, aina ya sera za lugha, na kuonesha namna sera ya lugha kama ilivyoingizwa katika Sera ya Utamaduni na Elimu. Data katika makala hii, kwa kiasi kikubwa, zimekusanywa kutoka maktaba na kwa wadau mbalimbali wa lugha. Changamoto zilizojadiliwa ni pamoja na: kutokuainishwa kwa mpango wa utekelezaji wa sera, sera ya lugha kushughulikia suala la elimu tu, na kutokupewa nafasi ya lugha nyingine za jamii. Mintarafu ya changamoto hizo, makala imebainisha sababu za changamoto hizo. Pia, imebainisha umuhimu kuhusu haja ya kuwa na sera madhubuti na mahususi ya lugha nchini Tanzania.

Downloads

Published

2021-10-05

How to Cite

Sovu, A. Y. (2021). CHANGAMOTO ZA UINGIZWAJI WA MASUALA YAHUSUYO LUGHA KATIKA SERA ZA ELIMU NA UTAMADUNI: HAJA YA KUWA NA SERA MAHUSUSI YA LUGHA TANZANIA. JARIDA LA MNYAMPALA, 2(1), 95–105. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/11

Issue

Section

ARTICLES