MAKOSA YA KISEMANTIKI YANAYOFANYWA NA WANAFUNZI WA KISWAHILI: MIFANO KUTOKA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI TEULE NCHINI RWANDA
Keywords:
Makosa, Semantiki, Makosa ya Kisemantiki, Wanafunzi, Kiswahili, Shule za SekondariAbstract
Makosa yanayojitokeza katika ujifunzaji wa lugha ya pili ni yale ya kifonolojia, kimofosintaksia, kisemantiki, na kiotografia (Corder, 1980; na Niyomugabo, 2016). Naye, Wray (2000) anaeleza kuwa katika uchunguzi wa makosa ya kilugha, baadhi ya tafiti zilizofanywa hazikushughulikia semantiki. Hivyo, makala hii inachanganua makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wa Kiswahili katika shule za sekondari nchini Rwanda. Malengo yake ni kubainisha aina za makosa ya kisemantiki yanayofanywa na kiwango cha makosa hayo yanavyoathiri umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili. Mbinu zilizotumiwa kukusanya data ni mahojiano, ushuhudiaji na uchambuzi matini. Data zilizokusanywa zilichambuliwa na kutolewa maelezo kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Uchanganuzi Makosa iliyoasisiwa na Corder (1967). Matokeo ya data zilizochambuliwa yalionyesha kuwa makosa ya kisemantiki yanayowakabili wanafunzi katika ujifunzaji wa Kiswahili yanasababisha changamoto za kisemantiki kwa wanafunzi Wanyarwanda katika ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili. Makosa yaliyobainishwa ni tafsiri kutoka lugha ya kwanza, makosa ya kimuundo, makosa ya kisemantiki leksia, kutumia sauti isiyofaa katika neno, makosa ya kutumia lugha ya kishairi na makosa ya kunukuu. Pia, makala imeonyesha kiwango cha wanafunzi cha kuathiriwa na makosa hayo. Kutokana na matokeo haya, imependekezwa kwamba ngazi mbalimbali zinazohusiana na ufundishaji na ujifunzaji ili kushirikiana kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto hiyo.