MCHANGO WA TEHAMA KATIKA UFUNDISHAJI WA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILLI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI TEULE WILAYANI NYAGATARE NCHINI RWANDA

Authors

  • Tulinumukiza Frodouard Chuo Kikuu cha Rwanda
  • Wallace K. Mlaga Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha

Keywords:

TEHAMA, Fasihi, Ufundishaji

Abstract

Makala hii inaangazia mchango wa TEHAMA katika ufundishaji wa fasihi andishi katika shule za sekondari wilayani Nyagatare, Rwanda. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uunganisho, ukitumia mbinu za usaili, ushuhudiaji, na uchanganuzi wa matini kukusanya data. Sampuli ilijumuisha wanafunzi 103, walimu wa Kiswahili 5 na wakuu wa masomo 5 walioteuliwa kwa usampulishaji lengwa. Data zilizokusanywa kwa usaili na uchanganuzi wa matini, zilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa madondoo na maelezo. Matokeo yameonesha kwamba TEHAMA huchangia pakubwa katika ufundishaji wa fasihi andishi. Inarahisisha upatikanaji wa nyenzo za kielimu kama vitabu vya kielektroni na video, huwezesha wanafunzi kuwasiliana na wenzao kimataifa, na kuwasaidia kujifunza stadi mpya. Aidha, TEHAMA huwapa wanafunzi motisha na kuifanya fasihi kuwa ya kuvutia zaidi. Hata hivyo, changamoto zilibainika, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa zana za kufundishia na mbinu duni za walimu. Ili kukabiliana na changamoto hizi, utafiti umependekeza maandalizi ya warsha za TEHAMA na kuboresha miundombinu shuleni. Matokeo haya yanaonesha umuhimu wa TEHAMA katika kuimarisha ufundishaji wa fasihi andishi na kutatua changamoto zilizopo.

Downloads

Published

2024-12-30

How to Cite

Frodouard, T., & Mlaga, W. K. (2024). MCHANGO WA TEHAMA KATIKA UFUNDISHAJI WA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILLI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI TEULE WILAYANI NYAGATARE NCHINI RWANDA. JARIDA LA MNYAMPALA, 4(1), 109–125. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/51

Issue

Section

ARTICLES