TATHIMINI YA SABABU ZA KUFANYIKA KWA MAKOSA YA KIMATAMSHI NA KIOTHOGRAFIA KATIKA KISWAHILI: MFANO WA SHULE TEULE ZA SEKONDARI WILAYANI NYARUGENGE NCHINI RWANDA
Keywords:
Makosa ya Kimatamshi, OthografiaAbstract
Makala imechunguza sababu za kufanyika kwa makosa ya kimatamshi na kiothografia katika lugha Kiswahili. Tafiti nyingi zilizofanyika zilijikita zaidi katika uchanganuzi wa makosa ya kimatamshi na kiothografia yanayofanyika katika Kiswahili bila kutoa sababu zinazosababisha makosa hayo. Kutokana na hayo, utafiti wetu ulitathmini vyanzo vya kufanyika kwa makosa ya kimatamshi na kiothografia miongoni mwa wanafunzi wanaosoma Kiswahili kama lugha yao ya pili. Makala iliongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Makosa iliyoasisiwa na Corder mnamo mwaka 1967. Sampuli ya watafitiwa ilihusisha walimu 6 wa Kiswahili na wanafunzi 15 kutoka shule teule tano tofauti. Shule hizi ziliteuliwa kwa kuwa zinakaa katika eneo lenye Waislamu wengi ambao ni wazungumzaji wakubwa wa Kiswahili. Shule hizo zilikuwa Gs. Camp Kigali, Gs. Cyahafi, Shule ya Kiufundi ya Leading, Lycée Notre Dame de Citeaux na Epa St Michel. Data zilikusanywa kwa kutumia mahojiano, ushuhudiaji na udurusu wa nyaraka. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa makosa ya kimatamshi na kiothografia katika Kiswahili yanatokana na ujuzi finyu wa lugha lengwa, kutojua kanuni za kisarufi, ukiukaji wa kanuni za kisarufi, uhamishaji wa vipengele vya lugha ya kwanza kwa lugha ya pili, wingilugha katika ujifunzaji wa Kiswahili pamoja na mtazamo hasi dhidi ya lugha ya Kiswahili.