CHANGAMOTO ZA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI WA KISWAHILI KAMA LUGHA YA PILI KATIKA SHULE ZA UPILI NCHINI RWANDA: MFANO WA SHULE TEULE WILAYANI MUSANZE
Keywords:
Ujifunzaji, Ufundishaji, Lugha ya Pili, Shule za UpiliAbstract
Makala hii inalenga kujadili changamoto zinazowakumba walimu na wanafunzi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya pili nchini Rwanda, mfano wa shule teule za upili wilayani Musanze. Aidha, makala hii iliongozwa na Nadharia ya Viwezeshi katika ufundishaji wa lugha iliyoasisiwa na Gibson katika mwaka wa 1977. Vilevile, wakati wa ukusanyaji wa data, mtafiti alitumia ushuhudiaji, usaili na uchanganuzi matini kama mbinu za kukusanya data. Walengwa walikuwa walimu na wanafunzi kutoka shule teule za G S Muhoza I na Ecole de Sciences de Musanze, wilayani Musanze. Data za watafitiwa zilifanyiwa uchanganuzi na matokeo yalibainisha kuwa walimu na wanafunzi wote hukumbwa na changamoto tofauti wakati wa ufundishaji wa Kiswahili. Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa nyenzo za kufundishia na kujifunzia, ujuzi finyu wa lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi, ukosefu wa mafunzo kwa walimu na mtazamo hasi wa wanafunzi kuhusu lugha ya Kiswahili. Makala, inapendekeza kuboresha ufundishaji wa Kiswahili nchini kwa kuchapisha vitabu vingi zaidi, kutoa mafunzo kwa walimu wa Kiswahili na kuongeza idadi ya vipindi vya Kiswahili. Pia, kuhakikisha kuwa Kiswahili kinatahiniwa katika mitihani ya taifa kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha tatu.