NAFASI YA JAZANDA KATIKA UWASILISHAJI WA MAUDHUI YA MAPENZI NA MAUMIVU YA KIHISIA: MIFANO KUTOKA WIMBO WA KIZA KINENE

Authors

  • Shadidu A. Ndossa Chuo Kikuu cha St John cha Tanzania

Keywords:

Jazanda, Maana Fiche, Muziki, Sanaa

Abstract

Makala hii inajadili matumizi ya jazanda katika wimbo wa Kiza Kinene wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Nandy, kwa kushirikiana na kundi la muziki la Sauti Sol kutoka Kenya. Kwa kutumia Nadharia ya Uhakiki wa Fasihi Jamii, makala inatathmini jinsi jazanda zinavyotumika kama mbinu ya kisanaa katika kuakisi mazingira halisi ya kijamii, kihisia na kiutamaduni ya wasanii na jamii zao. Aidha, makala inaonesha kuwa jazanda zilizopo katika wimbo huu zinahusiana na viungo vya mwili, mazingira ya asili, familia, biashara na imani za jadi, zikielezea kwa kina hisia za maumivu, upweke, usaliti na matarajio yaliyofifia katika mapenzi. Makala inahitimisha kuwa jazanda si mapambo ya lugha pekee bali ni nyenzo muhimu ya mawasiliano yenye mguso wa kijamii, kiitikadi na kihisia, inayomwezesha msanii kuwasilisha ujumbe mzito kwa namna ya ubunifu na isiyo ya moja kwa moja.

Downloads

Published

2024-12-30

How to Cite

Ndossa, S. A. (2024). NAFASI YA JAZANDA KATIKA UWASILISHAJI WA MAUDHUI YA MAPENZI NA MAUMIVU YA KIHISIA: MIFANO KUTOKA WIMBO WA KIZA KINENE. JARIDA LA MNYAMPALA, 4(1), 1–12. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/45

Issue

Section

ARTICLES