DHIMA YA TAFSIRI HIFADHI: UCHUNGUZI WA BIBLIA TAKATIFU

Authors

  • Rehema Stephano Chuo Kikuu cha Dodoma
  • Emanuel Samwel Kaghondi Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira

Abstract

Makala hii inafafanua dhima ya tafsiri hifadhi katika Biblia. Msingi wa makala hii ni kubainisha, kuchambua na kueleza dhima ya maneno ya lugha chasili ambayo yameendelea kuwapo katika Biblia hadi sasa. Maswali yanayoongoza makala hii ni mawili. Je, maneno yapi katika Biblia ni ya lugha chasili? Kwa nini maneno hayo yaendelee kuwapo katika lugha lengwa, hasa Kiswahili? Methodolojia ya utafiti huu ni uchanganuzi wa maneno yaliyopo katika tiniwayo katika Biblia: Maandiko Matakatifu toleo la mwaka 1997. Makala inabainisha kwamba tafsiri hifadhi ina dhima kubwa, hasa katika Biblia. Aidha, matokeo ya uchambuzi wetu yanaonesha kwamba tafsiri hifadhi, pamoja na dhima nyinginezo, inatunza utukufu wa Kimungu, historia na kumbukumbu ya mambo mbalimbali na kuonesha msisitizo wa mambo ya Kimungu. Kutokana na matokeo haya, makala hii inapendekeza kwamba, wasomaji wa tafsiri hifadhi wajijuvye vya kutosha kuhusu masalia ya lugha chanzi yaliyomo katika matini lengwa, hususani Biblia, ili waweze kuelewa ujumbe uliomo katika matini husika. Wasomaji hawa wataweza kujijuvya dhima za masalio yaliyopo katika maandiko kupitia kamusi, kusoma maandiko mengine yenye welekeo moja na kuwakabili wazungumzaji wa lugha chanzi.

Downloads

Published

2020-06-30

How to Cite

Stephano, R., & Kaghondi, E. S. (2020). DHIMA YA TAFSIRI HIFADHI: UCHUNGUZI WA BIBLIA TAKATIFU. JARIDA LA MNYAMPALA, 1(1), 38–49. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/33

Issue

Section

ARTICLES