KISWAHILI KATIKA MATAMASHA YA MAIGIZO YA SHULE NA VYUO NCHINI KENYA

Authors

  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi
  • Toboso Mahero Chuo Kikuu cha Alupe

Abstract

Matamasha ya shule na vyuo nchini Kenya huandaliwa kila mwaka kati ya Januari na Aprili. Matamasha haya hushirikisha kila shule na vyuo vya serikali pamoja na vya binafsi. Matamasha haya yalianzishwa mwaka wa 1959. Huu ulikuwa wakati wa ukoloni na kwa sababu hii, maigizo yalitawaliwa na sifa za matamasha na maigizo ya Uingereza yaliyoshirikisha taasisi za elimu ya juu. Matamasha ya mwanzo mwanzo nchini Kenya yalishirikisha taasisi za Wazungu na Wahindi pekee. Baada ya uhuru, matamasha haya yalianza kushirikisha shule na taasisi za Kiafrika. Ingawaje lugha za Kiafrika zimekubaliwa kushirikishwa katika tungo za kuwasilishwa katika matamasha haya, mawasilisho mengi huwa katika lugha ya Kiingereza. Hali hii imewacha Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika zikikosa kushirikishwa kikamilifu. Makala basi inajadili nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa taifa kupitia kwa matamasha haya.

Downloads

Published

2023-05-31

How to Cite

Kandagor, M., & Mahero, T. (2023). KISWAHILI KATIKA MATAMASHA YA MAIGIZO YA SHULE NA VYUO NCHINI KENYA. JARIDA LA MNYAMPALA, 3(1), 122–133. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/25

Issue

Section

ARTICLES