UCHANGANUZI WA MAKOSA YA MSAMIATI WA KISWAHILI KATIKA MATINI ANDISHI ZA HABARI: MFANO WA BBC SWAHILI NA DW KISWAHILI

Authors

  • Alcheraus R. Mushumbwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Abstract

Makala hii imechunguza makosa ya msamiati yanayofanyika katika vyombo vya habari vya BBC Swahili na DW Kiswahili. Istilahi msamiati, katika makala hii, inatumika kwa maana ya maneno yote yanayotumika katika lugha (TATAKI, 2013:384 na BAKITA, 2015:701). Malengo ya makala ilikuwa ni kuchanganua makosa ya msamiati, kubainisha sababu za makosa ya msamiati na athari za makosa hayo katika lugha. Ili kutimiza madhumuni ya Makala hii, kiunzi cha uchanganuzi wa habari kiisimu (van Dijk, 1988) kilizingatiwa. Sampuli ya utafiti huu ilihusisha matini ishirini za habari zilizosomwa kutoka kwenye tovuti za vyombo vya habari vilivyochunguzwa. Matokeo ya uchunguzi wa makala inaonesha kuwa vyombo vya habari vya BBC na DW (Idhaa za Kiswahili) hufanya makosa yanayohusu msamiati wa Kiswahili katika kuripoti habari kwa maandishi. Makosa hayo ni uunganishaji na utenganishaji wa maneno, uchopekaji na udondoshaji wa vipashio vinavyounda maneno, matumizi ya neno lisilofaa na utohozi wa maneno. Vilevile, makala ilibaini kwamba makosa hayo yalisababishwa na umilisi hafifu wa msamiati wa Kiswahili; athari ya lugha ya mazungumzo na lugha za kigeni. Mwisho, makala ilibaini kuwa makosa hayo yana athari kwa watumiaji wa Kiswahili na kupendekeza namna ya kuyaepuka.

Downloads

Published

2023-05-31

How to Cite

Mushumbwa, A. R. (2023). UCHANGANUZI WA MAKOSA YA MSAMIATI WA KISWAHILI KATIKA MATINI ANDISHI ZA HABARI: MFANO WA BBC SWAHILI NA DW KISWAHILI. JARIDA LA MNYAMPALA, 3(1), 54–71. Retrieved from https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/21

Issue

Section

ARTICLES