WITO WA MAKALA

2025-09-23

KITIVO CHA INSIA NA ELIMU

JARIDA LA MNYAMPALA

https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/libraryFiles/downloadPublic/1

Jarida la Mnyampala (JM) ni jarida la kitaaluma lililo chini ya Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha St John cha Tanzania. Jarida linachapisha makala za Isimu, Fasihi na Utamaduni wa Kiswahili.

Kwa mara nyingine tena, Mhariri Mkuu anawakaribisha wapenzi, watafiti na wataalamu wa lugha ya Kiswahili kuwasilisha makala kwa ajili ya Juzuu Na. 5 linalotarajiwa kuchapishwa mwanzoni mwa mwaka 2026.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa makala:

  1. Iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  2. Iwe na maneno kati ya 3000-5000, ikiwamo ikisiri isiyozidi maneno 200.
  3. Ipigwe chapa katika programu ya word na nafasi ya 1.5 kati ya mstari na mstari.
  4. Urejeleaji ufanywe kwa kutumia mtindo wa APA toleo la 6.
  5. Ihaririwe vizuri.
  6. Ukurasa wa kwanza wa makala ujumuishe taarifa za mwandishi kama vile jina kamili,
  7. anuani, baruapepe, namba ya simu, asasi au taasisi alipo.
  8. Makala zote zitumwe kwa Mhariri Mkuu kupitia baruapepe jaridalamnyampala@sjut.ac.tz
  9. Tarehe ya mwisho ya kupokea makala ni 31 Oktoba 2025.
  10. Makala ambayo haitazingatia maelekezo haitafanyiwa kazi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu jarida tembelea tovuti yetu

https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala au kupitia ukarasa wa Ajol https://www.ajol.info/index.php/jm

Mhariri Mkuu,

Jarida la Mnyampala,

8 Agosti 2025.