TY - JOUR AU - Maitaria, Joseph N. PY - 2021/10/05 Y2 - 2024/03/29 TI - HADHIRA YA USHAIRI HURU WA KISWAHILI NI IPI? JF - JARIDA LA MNYAMPALA JA - JM VL - 2 IS - 1 SE - ARTICLES DO - UR - https://journals.sjut.ac.tz/index.php/mnyampala/article/view/8 SP - 32 - 46 AB - <p style="text-align: justify;">Makala hii inaangazia mustakabali wa hadhira katika upokezi wa   ushairi huru wa Kiswahili. Mwanzoni mwa miaka 1970, ushairi huu   ulijitokeza kwa kasi na ulituhumiwa kwa kutozingatia arudhi za   kimapokeo. Watunzi wa awali wa ushairi huu walikuwa wataalamu   wa lugha na wahakiki wa fasihi; waliotoa maelezo muhimu kuhusu   dhana na sifa za ushairi wa Kiswahili. Kabla ya miaka 1960, ushairi   wa kimapokeo ulikuwa umesambaa na umezoewa katika jamii.   Kujitokeza kwa ushairi huru kulisababisha watunzi na hadhira   kugawanyika katika makundi: lile linalojinasibisha na arudhi, lile   lisilojinasibisha na arudhi, na lile linalojinasibisha kwa kiasi na   arudhi hizo. Katika miaka ya 1970, waliouendeleza zaidi ushairi huru   walikuwa ‘vijana’ waliobahatika kupata elimu ya juu katika taaluma   ya fasihi na walitarajia kuchangia katika ufafanuzi wa dhana na sifa   za ushairi wa Kiswahili kwa ujumla. Swali linalofafanuliwa katika   makala hii ni: kwa nini ushairi huru wa Kiswahili ni kivutio cha   wataalamu wa lugha na wahakiki wa fasihi? Nadharia ya Semiotiki   imetumika kufafanulia matini za lugha kama viishara na viashiria   vinavyohitaji kufasiriwa. Data ya uchanganuzi ilitokana na upitiaji   wa mashairi katika diwani teule za mashairi ya Kiswahili. Aidha, data   nyingine ilitokana na usaili na hojaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na   wataalamu wa lugha na fasihi.</p> ER -